KELVIN SABATO NDANI YA TIMU YA TAIFA

Mshambuliaji wa Majimaji ya Songea ambaye ni maarufu pia kwenye mashindano ya Ndondo Cup, Kelvin Sabato ameitwa kukiongezea makali kikosi cha Taifa Stars.

Baada ya kutoka Afrika Kusini kushiki michuano ya Cosafa ambayo imeshika nafasi ya tatu,Taifa Stars itakuwa na kibarua cha kuwania nafasi ya kucheza michuano ya CHAN dhidi ya Rwanda Julai  15.

Sabato amefurahia kuitwa kwake na kusema ni sehemu ya ndoto yake kuichezea timu ya Taifa pia nyota huyo amegusia kucheza kwake Ndondo.

“Ligi zimekwisha nahitaji kuendelea kuwa fiti kama mchezaji, nadhani sio kitu kibaya kucheza Ndondo maana nimekulia katika mazingira ya soka hilo.

“Nimefurahia sana kuitwa timu ya Taifa na nitajitahidi kuonyesha kuwa Mayanga hajakosea kuniongeza kwenye kikosi chake,” alisema Sabato.

Sabato aliyekuwa akihusishwa kujiunga na Simba kipindi hiki cha usajili anaichezea timu ya Stimutosha ambayo imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora katika mashindano ya Ndondo Cup.

No comments

Powered by Blogger.