Stars mshindi wa tatu kombe la Cosafa.

Timu ya taifa tanzania Taifa Stars imefanikiwa kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Cosafa baada ya kuichapa Lesotho kwa mikwaju ya penalti.

Stars imeibuka na ushindi wa mikwaju 4-2 dhidi ya Lesotho baada ya dakika 90 kumalizika 0:0

Katika michuano hiyo inayopigwa nchini Afrika Kusini, Shiza Kichuya ndiye aliyekuwa wa kwanza kupiga penalt na mpira kugonga mtamba wa panya (swinger post)na kukosa penalty hio.
Matumaini ya watanzania yakiwa yamefifia kutokana na kukosa kwa penalti hio ya kwanza  baadaye Lesotho walipoteza penalti mbili, moja ikigonga mwamba na nyingine kipa Said Mohamed ‘Nduda’ akikoa moja.
Waliofunga upande wa Stars ni Himid Mao, Simon Msuva, Abdi Banda na Raphael Alpha aliyema malizia kazi.
Ushindi huu unakuja siku 25 baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 Juni 10, mwaka huu katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi L kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Tanzania inaondoka na dola za Kimarekani 10,000 zaidi ya Sh. Milioni 22 kwa fedha za nyumbani, wakati Lesotho wamepata dola 8,300.
Fainali ya COSAFA Castle 2017 itachezwa Jumapili Uwanja wa Royal Bafokeng, Phokeng mjini Rusternburg baina ya majirani, Zambia na Zimbabwe na bingwa atapata dola 42,000 na mshindi wa pili dola 21,000.

No comments

Powered by Blogger.