CARRICK KUVAA KITAMBAA CHA UNAHODHA UNITED

Wayne Rooney anatarajiwa kutua Everton majira ya joto, na nafasi yake ya unahodha inaweza kuchukuliwa na Michael Carrick akisaidiana na Herrera
Imeripotiwa Jose Mourinho atampa kitambaa cha unahodha Michael Carrick katika kampeni za msimu wa 2017/18, Manchester United inapojiandaa na maisha bila ya Wayne Rooney.
Nahodha huyo wa muda mrefu wa United anatarajiwa kujiunga na klabu ya utotoni Everton siku chache zijazo, hivyo atahitimisha kipindi cha miaka 13 alichodumu Old Trafford - ambapo mitatu katika hiyo amekuwa kiongozi dimbani.

No comments

Powered by Blogger.