CAZOLA HATI HATI KUTOKUICHEZEA ARSENAL...

Nyota wa Arsenal Santi Cazola huenda akawa amecheza mechi yake ya mwisho katika klabu hiyo kufuatia ripoti kuwa amepata majeraha mapya.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 hajatokea kwenye kikosi cha Washika Mtutu wa London tangu Oktoba alipopata majeraha ya tendoni za mguu katika mechi za Ligi ya Mabingwa.

Tangia hapo, kiungo huyo amepata tiba kadhaa za upasuaji, lakini kumekuwa na sintofahamu ni lini atarejea katika uzima wake.

Sasa, The Express kimeripoti kuwa Cazorla anaweza kuwa nje ya dimba kwa misimu miwili kamili, jambo linalomaanisha kuwa anaweza asicheze tena Arsenal kabla ya mkataba wake kufika tamati majira ya joto 2018.

Ingawa, kama hatapata majeraha yoyote mapya, anaweza kurejea dimbani akiwa na kikosi cha umri chini ya miaka 23 Aprili mwakani.
Kiungo huyo alisaini mkataba mpya msimu uliopita.

No comments

Powered by Blogger.