TANZANIA KUTUPA KARATA YAKE HI LEO DHIDI YA ZAMBIA
Timu ya taifa ya Tanzania wapo kwenye Mechi ya Nusu Fainali ya COSAFA CUP ambayo watacheza na Zambia huko Moruleng Stadium hii leo
Tanzania wametinga Nusu Fainali baada ya Juzi kuwabwaga Wenyeji South Africa 1-0 kwa Bao la Dakika ya 18 la Elias Muguli wakati Zambia wakiitoa Botswana 2-1 kwenye Mechi za Robo Fainali.
Nusu Fainali nyingine ambayo itachezwa hii Leo baada ya Mechi ya Tanzania ni kati ya Lesotho na Zimbabwe.
Wakati Timu zilizoshinda Robo Fainali zikitinga Nusu Fainali, Timu zilizopteza Hatua hiyo zipo kinyang’anyiro cha kugombea Ngao ,na Jana South Africa waliifunga Botswana 2-0 na kutinga Fainali
Hii ni mara ya 3 kwa Tanzania kucheza Mashindano haya baada ya kushiriki yale ya 1997 na 2015.
Nchi Wanachama wa COSAFA, South Africa, Swaziland, Botswana na Zambia waa Wenyeji South Africataanzia Hatua ya Robo Fainali ambapo South Africa itacheza na Mshindi wa Kundi A na Swaziland kucheza na Mshindi wa Kundi B wakati Botswana ikivaana na Zambia.
Mashindano ya COSAFA yalianzishwa Mwaka 1997 na Nchi za South Africa, Zambia na Zimbabwe kubeba Kombe mara 4 kila moja wakati Angola ikibeba mara 3 na Namibia mara 1.
NUSU FAINALI - KOMBE
05/7 19 Zambia vs Tanzania, 17h00, Moruleng Stadium
05/7 20 Lesotho vs Zimbabwe, 19h30, Moruleng Stadium
FAINALI - NGAO
07/7 21 South Africa vs Winner M18, 17h00, Moruleng Stadium
MSHINDI WA 3
07/7 22 Loser M19 vs Loser M20, 19h30, Moruleng Stadium
FAINALI - KOMBE
09/7 23 Winner M19 vs Winner M20, 15h00, Royal Bafokeng Sports Palace
Leave a Comment