TETESI MBALI MBALI ZA USAJILI
LEMAR AKUBALI £90K KUTUA ARSENAL

Arsenal wamefikia makubaliano ya ujira wa £90,000 kwa wiki na Thomas Lemar, lakini bado wanahitaji kufikia makubaliano na Monaco kumsajili winga huyo, kwa mujibu wa The Sun .
Imeripotiwa kuwa dau la euro milioni 45 kwajili ya Lemar limekataliwa na Monaco, ambao hawana haraka ya kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.
CEBALLOS ATIMKIA MADRID KWA €18M

Dani Ceballos amekubali mkataba wa miaka sita kujiunga na Real Madrid na yupo mboni kukamilisha uhamisho kwa euro milioni 18, kwa mujibu wa Marca .
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 alikuwa akifuatiliwa na Barcelona, lakini anependelea kujiunga na Real Madrid.
RUDIGER AKARIBIA KUTUA CHELSEA

Uhamisho wa Antonio Rudiger kutoka Roma kwenda Chelsea unakaribia kukamilika, wakala wake ametua Uingereza kumaliza mchakato huo, kwa mujibu wa Sky Sports .
ARSENAL YAMBANIA ALEXIS KUONDOKA

Arsenal wameweka wazi kuwa hawana mpango wa kumuuza Alexis Sanchez wala Alex Oxlade-Chamberlain kwa wapinzani wao wa Ligi Kuu Uingereza, kwa mujibu wa Daily Star .
Manchester City walikuwa wakiongoza katika mbio za kumsajili Sanchez, wakati Oxlade-Chamberlain alikuwa akihusishwa na klabu ya Liverpool.
COSTA AKARIBIA KUTUA JUVENTUS

Kiungo wa Bayern Munich Douglas Costa anakaribia kukamilisha uhamisho wa mkopo kutoka Ujerumani kutua Juventus na fursa ya kutua kwa mkataba wa kudumu wa euro milioni 40, kwa mujibu wa La Stampa
Leave a Comment