VALVERDE HANA MPANGO NA WACHEZAJI WAPYA BARCA

 Barcelona inaweza kumtoa Ivan Rakitic ili imnase Mchezaji wa Kimataifa wa Italy Marco Verratti.
 Kocha Mkuu mpya wa Klabu hiyo Ernesto Valverde amedai hana wasiwasi na Kikosi kilichopo Kwa sasa ,Valverde amesema itakuwa vema kama  wakisaini Wachezaji wapya lakini yeye ana furaha kufanya kazi na Wachezaji walioko katika kikosi hicho .

Ripoti kutoka Spain zimedai Barca iko tayari kuwatoa Ivan Rakitic au Andre Gomes ili kuweka nguvu zaidi kumpata Verratti kutoka Paris Saint-Germain.

Inadaiwa Barca iko tayari kumtoa Rakitic pamoja na Euro Milioni 65 kwa PSG ili impate Verratti.
Lakini Valverde amesisitiza wote, Rakitic na Gomes, bado wanahitajika hapo Nou Camp.
Ameeleza: "Wote hao ni Wachezaji wangu na wamo kwenye mipango yangu!"

No comments

Powered by Blogger.